HUU NDIO UKWELI:..TABIA MBAYA NA VINYONGO VYA MAWIFI VYAMKERA SANA CATHY WA BONGO MOVIE....

0
Msanii mkongwe wa filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’
MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa anakerwa na tabia za mawifi kuwachukia wake za kaka zao bila sababu za msingi.
Akichonga na paparazi wetu, Cathy alisema mawifi wengi huwachukia na kuwawekea vinyongo wake wa kaka zao hata kama hawajawakosea, kitu ambacho kinamkera na anaamini siyo yeye peke yake, bali jamii nzima inachukia tabia hizo. 

“Ukweli nakerwa sana, yaani utakuta wanakuchukia bila sababu, muda mwingine wanakuwa na vinyongo mioyoni na kusema maneno yasiyofaa ya kukuponda, hawajui kwamba nao ni binadamu kama walivyo wao, naomba waache tabia hii, siyo nzuri,”alisema.

0 comments:

Tafadhali LIKE page yetu Upate habari mpya kwenye Facebook yako.BOFYA LIKE

Powered By Kandili Yetu Team